Shared Stories




Huwa imezoeleka kuwa sikukuu ndizo siku za kufurahi baada ya siku nyingi za mahangaiko, watu hukutana na kukaa pamoja, kubadilishana mawazo, kutafakari nini kifanyike na kwa namna gani, lakini hata hivyo wapo ambao hutumia siku hizi sa sikukuu kinyume na dhana ya siku zenyewe.
Ni wazi kabisa kuwa sikukuu zimekuwa zikitumiwa sana hasa na vijana ili kujifurahisha pale wanapokutana aidha na wapenzi wao, au wengine huchukulia kama ndiyo nafasi ya kutoka na kufanya kitu ambacho alikuwa anatamani kukifanya ila alikuwa hapati nafasi ya kutoka, tumekuwa tukishuhudia matukio mengi na mabaya hasa kipindi cha sikukuu, mfano mtu kafumaniwa na mke au mume wa mwenziwe, au utakuta mara baada ya sikukuu kupita dada zetu huwa wanajikuta kuwa wana ujauzito na hata pengine wengine hujikuta wamepata maamukizo ya magonjwa ya zinaa likiwemo ukimwi kisa tu alijiachia siku ya sikukuu alipopata ruhusa ya kwenda kutembea.
Ni vyema kama tutakuwa tunatambua nini maana ya sikukuu halafu tukatambua umuhimu wake na athari zake kwetu ili basi tuweze kuepukana na dhana ya kupeana apointment za kufanya ngono na mambo mengine machafu siku za sikukuu mfano Pasaka, krismasi na nyinginezo. Tujitambue, tujithamini, tujipende, tujijali na hata wenzetu pia.
Siku moja hugharimu maisha yote.

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.