Mkutano wa vijaa wa UN Tanzania kufanyika mjini Dodoma

Hivi ndivyo mkutano ulivyokuwa umelenga 
Ni mkutano uliowajumuisha vijana mbalimbali kutoka mikoa yote nchini kwa dhumuni la kujadili matatizo mbalimbali yanayozikumba nchi zinazoendelea hasa katika swala zima la maendeleo na kuandaa maadhimio yatakayoziwezesha nchi hizi kufikia kile kinachosemekana kuwa ni maendeleo endelevu.


Mkutano huo ulifanyikia mjini Dodoma katika ukumbi wa zamani wa Buge la Jamuhuro ya muungano wa Tanzania alimaarufu kama ukumbi wa Pius Msekwa. Mkutano huo ulifunguliwa na naibu spika wa bunge la jamuhuri ya muungano Mh. Job Ndugai ambapo ulidumu kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe 31, Machi hadi tarehe 3, April 2012.

hata hivyo baada ya mkutano huo vijana hao walifanya marekebisho ya katiba ya asasi hiyo pamoja na uchaguzi wa viongozi wa YUNA taifa baada ya walio kuwepo kumaliza muda wao wa mwaka mmoja.

Picha ya pamoja kati ya washiriki wa mkutano huo na Mgeni rasmi, naibu spika wa bunge la jamuhuri ya muunganowa Tanzania Mh. Job Ndugai


Ukumbi wa zamani wa bunge alimaarufu kama Pius Msekwa abapo mkutano ulifanyikia

Huyu ni mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo ambapo alikuwa anasoma ripodi ya nchi ambayo alikuwa anaiwakilisha

 Hawa pia ni baadhi ya washiriki wa mkutamo huo
 Vijana wa Tanzania wanayo nafasi kubwa katika kuibadilisha dunia kama wataendelea kwa umoja ambao wanao kama inavyoonekana hapa

Hawa ni washiriki na wawakilishi wa Uganda wakijaribu kuandaa maadhinio kwa ajili ya mkutano huo kwa nchi yao.

Raisi wa YUNA Tanzania bwana Adam Antony akiwa anaongea na washiriki wa mkutano huo


Hapa washiriki wakiwa wanakula chakula kwa pamoja huku wakiwa na furaha


Picha ya Viongozi wastaafu pamoja na baadhi ya vijana waliohidhuria mkutano

Sikuishia tu kuhudhuria mkutano, bali nilikutana na watu mbalimbali na kupata marafiki wengi, huyu ni mmoja wao bwana Exavery Kigosi kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam. Ukweli aliyekosa MUN 2012 amekosa mengi



Kwakweli timu ya maandalizi ilifanya kazi kubwa sana na wanahitaji pongezi, mambo ya chakula ukwaeli yalikuwa safi sanaaaaaaa!!!!!!!!


Ni wakati wa mkutano ambapo nilikuwa nazungumzia mambo mbalimbali kuhusu nchi yangu ya uwakilishi ambapo nilikuwa nawakilisha Uganda


Hapa ni katika usiku wa utamaduni ambapo washiriki wa mkutano walikuwa wakicheza na kufureahia kwa pamoja

Hawa ni viongozi wapya wa YUNA Tanzania ambao walichaguliwa waada ya kumalizika kwa mkutano wa taifa wa vijana wa UN

Hii ni picha ya pamoja akiwepo mimi kushoto bi Hadija Hassan anayefuatia pamoja na rafiki yetu tuliye hudhuria mkutano huo pamoja

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.