TANZANIA TUMRUDIE MUNGU
Kwa miaka mingi tumekuwa tukisikia kuwa Tanzania ni nchi ya amani na watu wake ni wenye upendo, ukarimu na unyenyekevu kwa wageni na hata wenyeji.
Ila kitu cha kusikitisha, kwa sasa amani imebaki midomoni mwa watu tu, tumegeuka wanyama, tunauana bila hata huruma, tunawaua vichanga wasio na hatia, sijui wapi tunakwenda jamai, ewe mama, ewe nesi na wewe daktari, unamjua Mungu au unamsikia tu?
Ukweli tukio la hao vichanga zaidi ya kumi waliouwawa kinyama na kutupwa linatuashiria ni watanzania?
Hebu tujiulize kuwa kama nasi tungefanyiwa hivyo tungekuwa wapi sasa? Swala la kufanya starehe za ngono ni la mtu binafsi lakini kama ulikuwa huhitaji kuzaa kwanini uruhusu kushika mimba?
Mimi naomba serikali sasa ichukue jitihada za makusudi kuhakikisha kila kiumbe anapata haki yake ya kuishi kama ilivyo kwenye katiba.
Na kuhusu hiyo hospitali inayoshukiwa, uchunguzi ufanyike kwa makini bila kuingiza siasa ndani yake na hatua za nidhamu na za kisheria zichukuliwe, tumechoka kusikia habari za Hospitali ya Mwananyamala, kama uendeshwaji wake umeshindikanda ni bora kuifungia kuliko kuendelea kushuhudia matendo ya kinyama yakiendelea katika nchi yetu hususani hospitali ya Mwananyamala.
No comments
Thank for your coment