KILE KITAKACHO TUPONZA WATANZANIA

Ni muda mrefu sana toka Tanzania ijipatie uhuru wake, pamoja na misukosuko ambayo tulipitia hatuna budi kumshukuru Mungu, amani imekuwa ndiyo sifa kubwa ya nchi hii katika mataifa mbalimbali duniani, hili limetupelekea kwa namna moja ama nyingine kuendelea kiuchumi kupitia sekta ya utalii ambayo kwa sasa ndiyo sekta kuu ya pili kuliingizia taifa mapato.
Lakini wasiwasi unazidi kuendelea pale ambapo yanatokea mambo mbalimbali ambayo kwa namna moja ama nyingine yamekuwa yakituharibia sifa yetu kuu ya kuwa kisiwa cha amani.
Jambo linalonisikitisha zaidi ni pale ambapo watanzania wenyewe tumekuwa mstari wa mbele kuchochea kupoteza sifa yetu hii kuu
Kwnza kabisa ningependa kuanza na vyombo vya habari ambavyo kwa namna moja au nyingine vina mchango mkubwa sana katika kudumisha amani au hata kuipoteza amani.
Kwa siku kadhaa sasa tumekuwa tukishuhudia wamiliki wa mitandao mbalimbali ya kijamii wakiandika habari kuhusu kuwepo ma mgogro kati ya Tanzania na Rwanda, ikiwemo kutoa kauli ambazo kimsingi hazijulikani kuwa vyanzo vyake ni vipi.
Ni kweli kuwa kila mtu ana wajibu wa kupata taarifa na kupokea taarifa bila kuzuiwa, lakini pia lazima uwepo utaratibu mzuri wa utoaji wa taarifa hizo, la sivyo yanaweza kutukuta yale ambayo yaliwapata majirani zetu Kenya mwaka 2007/2008 ambapo vyombo ya habari vilikuwa na mchango mkubwa sana katika mgogoro ambao uligharimu maisha ya watu wengi.
Mtazaomo wangu ni kwamba, kama hakutakuwa na udhibiti katika swala zima ta utoaji wa habar basi tusubiri kwa muda usio mrefu na tutajikuwa katika wakati ambao hakuna hata mmoja wetu anautegemea wala kuupenda.
Wito wangu kwa Serikali, Vyombo vya habari na Wamiliki wa mitandao hii ya kijamii zikiwemo blogs:
  1. Tufanye uchunguzi kwanza kwa habari tunazotaka kuzitoa kwa uma ili kuepusha kuwachanganya wananchi ambao kwa namna moja ama nyingine hatuujui ukweli wa mambo.
  2. Serikali kupitia wizara ya mambo ya habari na mawasiliano iweke utaratimu maalumu wa utoaji na uandikaji wa taarifa katika blog na mitandao mbalimbali ya kijamii.
  3. Swala zima la utoaji wa kuhusiana na maswala yanayoigusa nchi ziachwe chini ya wizara husika na sio mtu mmoja mmoja kuandika tena vitu ambavyo havina uthibitisho wala uchunguzi wowote.
  4. Mwisho kabisa napenda kuwasihi watanzania kuacha kushabikia maswala linalohisinana na migogoro, tunatakiwa tujue kwamba zipo sehemu ambazo wanatamani japo kupata amani ya siku moja tu wakapata muda wa kukaa pamoja na familia zao lakini kutokana na machafuko yalitopo inakuwa vigumu sana.
Tukumbuke kwamba kuipoteza amani linaweza kuwa swala la siku moja tu lakini kuirudisha tena likatugahrimu maisha yetu yote.
Ningependa kuona kama sisi tungejifunza kupitia majirani zetu ambao wameshapitia katika machafuko na wale ambao bado wapo katika machafuko, kupitia wao tuone ni namna gani tutaidumisha amani katika nchi yetu Tanzania.
Mimi binafsi naipenda sana nchi yangu Tanzania, najivunia sana kuzaliwa katika nchi hii japokuwa yapo mapungufu mbalimbali yanayotukabili, hii hainifanyi kuwa mmoja wa wale wanaoitakia mabaya nchi yangu, ningependa na nitafurahi sana kama watanzania wote tungeungana na kuitakia amani nchi yetu ikiwemo kuiombea na kuwapinga vikali wale ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa wanachochea katika kuipoteza amani yetu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu tubariki watanzania, amani iwe chetu cheo, fujo kuzikwepa, kwa upendo na mshikamano kuishi na udugu wetu wa enzi kuuenzi

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.