HOSPITALI YA MKOA DODOMA NI TISHIO



Hii ni wodi namba Nne katika Hospitali ya mkoa wa dodoma ambapo mimi mwenyewe nilifika nikiwa na mgonja wangu tukiwa tumepata transifer kutoka katika hospitali ya Chuo cha Dodoma, ila nilichokikuta huku kilikuwa ni kinyume na matarajio kwani mazingira yalikuwa machafu kiasi kwamba sio kuwa ni magumu tu bali pia ni hatari kwa afya za wagonjwa, huduma hazikuwa za kuridhisha pia shuka na vyandarua vilikuwa vichafu kiasi kwamba kwa mda kidogo niliokaa wodini hapo nilishikwa na mafua, je wagonjwa ambao hushinda na kulala humo zaidi ya wiki? Sijui kama tunaponya au twaua, serikali inabidi kufanya jitihada kukabiliana na tatizo hilo, kwa hospitali kubwa kuwa na hali kama hii ni uzembe usio vumilika, tuwapende wagonjwa.

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.