MIAKA 50 (HAMSINI) YA UHURU TANZANIA TUNAKWENDA WAPI?
Ni hivi karibuni tu tutakuwa tunashuhudia sherehe za kutimiza
miaka hamsini toka kupatikana kwa uhuru wa Tanzania mnamo Desemba 9,
1961, kutoka katika ukoloni wa Waingereza, hizi ni sherehe muhimu sana
ukizingatia hii ni nusu karne tangu kupatikana kwa uhuru, umri wa mtu mzima
ambaye kama ameoa basi ana familia yenye watoto, wajukuu na hata
vitukuu.
Ni haki yetu kufurahi na kusherehekea kwa kila njia tukio hili
muhimu katika historia ya Tanzania, tukio ambalo kwalo tunakumbuka kitendo cha
nchi yetu kuwa huru katika nyanja mbalimbali, ikiwemo uhuru wa kujitawala,
uhuru wa kuamua nini cha kufanya, uhuru wa kuchagua nani rafiki na kumtambua
nani ni adui, uhuru wa kuamua na kutambua njia zilizo bora kwa nchi na wananchi
wake.Tumeshuhudia awamu nne za uongozi tangu kupatikana kwa uhuru, tukianzia na
muasisi wa taifa hili tukufu ambalo pia ni kisiwa cha amani, yaani baba wa
taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye aliliongoza taifa tangu
kupatikana kwa uhuru hadi miaka ya 1980, ambapo katika kipindi chote hicho
tulishuhudia jitihada mbalimbali ambazo alizifanya mwalimu ikiwemo kupambana na
swala la ukoloni mamboleo, kupiga vita swala zima la uhujumu uchumi ikiwemo
kuwachukulia hatua kali wale waliobainika kujihusisha na uhujumu
uchumi, kuwaunganisha wananchi wote bila kujali dini, kabila au itikadi zao.
Hiki kilikuwa kipindi kigumu sana katika uongozi kwani lilikuwa ni jukumu la
mwalimu kuhakiisha kila mwananchi anapata mahitaji muhimu ikiwemo huduma za
kijamii. Pia katika kipi hiki tulishuhudia mapambano dhidi ya uvamizi wa nchi
yetu uliofanywa na nduli Idd Amin Dada, hata hivyo Mwalimu alihakikisha anawalinda
wananchi na mali zao likiwa kama jukumu lake kwa kupambana na Amini
hadi alipouchukua ushindi. Hiki kilikuwa kipindi kigumu sana, lakini kwa
jitihada za mwalimu tuliendelea mbele katika kujiletea maendeleo.
Kikaja kipindi cha pili ambacho kilikuwa chini ya raisi Ali Hassan Mwinyi, kuanzia miaka ya 80 hadi kufikia mwaka 1995. Hiki nacho kilikuwa na mambo yake, tulishuhudia kuanzisha kwa sera mbalimbali zikiwemo biashara huria, ubinafsishaji wa mali ya umma, uwekezaji pia ikiwemo sera ya vyama vingi.Haya yalikuwa mabadiliko makubwa sana yaliyo chukua nafasi kwa hipindi hiki.
Kipindi cha tatu ni kuanzia miaka ya 1995-2005, ambacho kilikuwa chini ya Mh: raisi Benjamin Willium Mkapa ambapo pia katika kipindi hiki kulikuwepo na mabadiliko kadhaa katika harakati za kutaka kujikwamua kiuchumi, kwa mfano kubadilishwa kwa sera ya nje kuwa za kiuchumi (economic foreign policy) ambapo sasa sera yetu ya nje inasisitiza mahusiano ambaya ni ya kiuchumi zaidi kuliko siasa.
Na awamu ya mwisho ambayo ndiyo ya nne ni hii ambayo ndani yake tunakwenda kuadhimisha kutimiza miaka hamsini tangu kupatikana kwa uhuru wa Tanzania, ni kipindi ambacho kiko chini ya raisi Jakaya Mrisho Kikwete, ambacho kimeanzia 2005 na ambacho kitakwenda hadi mwaka 2015.Basi tukiwa tunaelekea katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanzania inatubidi tutafakari kule tulikotoka, mambo na changamoto ambazo tumepitia, hatua ambayo tumepiga katika swala zima la maendeleo na nini matarajio yetu ya baadae.Hata hivyo pia tunatakiwa kujiuliza maswali kadhaa ili kujihakikishia kuwa kile tunachokwenda kukifanya kina umuhimu gani na usahihi gani, kwanza tunatakiwa tujiulize nini maana ya uhuru? Je uhuru uko kwa ajili ya nani? Je uhuru tulio nao ndio uhuru tuliokuwa tunauhitaji? Kuna faida gani kuwa na uhuru? Je uhuru tulio nao unawafaidisha wanajamii wote au tabaka fulani ambalo lilo madarakani? Je kuna athari gani za kuuchezea uhuru tulio nao?.....Haya ni baadhi tu ya sehemu ya maswali hayo. Hata hiyo inawezekana kuwa kwa walio wengi, uhuru ni kile kitendo cha kutotawaliwa na taifa jingine, hii ni kweli, lakini maana hii imeangalia sehemu tu ya maana ya uhuru.Kwa maana ndogo tu "Uhuru ni kitendo cha nchia au hata mtu kuwa na maamuzi binafsi ya nini cha kufanya, lini, wapi, namna gani, na kwa manufaa ya nani bila kuingiliwa na mtu au taifa jingine lolote" hata hivyo uhuru huo hugusa nyanja mbalimbali za maisha kama vile siasa, utamaduni, jamii na hata mila na desturi.Hata hivyo inaonesha kuwa pamoja na kuwa Tanzania inatimiza miaka hamsini ya uhuru, lakini hakuna uhuru wa kweli bali uhuru ulio wa bendera ambao hauna faida yoyote kwa wanajamii wa Tanzania. Naomba kutonukuliwa vibaya bali kuchambua kwa kina na kupata kiini cha ukweli. Hii inamaana kuwa, japo tunasema kuwa tuna uhuru, uhuru huo uko mikononi mwa watu wachache ambao wanaishikilia nchi hii....Hili linadhihirika waziwazi pale tunapowaona waheshimiwa wabunge ambao tumewapa dhamana ya kutuwakilsha serikalini wamekuwa waking'ang'ania kujilimbikizia posho ili hali wananchi majimboni wanaangamia kwa njaa, ukosefu wa maji, huduma mbovu za kijamii, magomjwa yasizotibika, na vifo visivyo na msingi..... Hili linawapa wasiwasi wananchi juu ya serikai tuliyo nayo. Pia katika kipindi hiki tumekuwa tukishuhudia migomo na maandamano katika sehemu mbalimbali humu nchini. Jambo la kusikitisha zaidi ni pale serikali inapotumia nguvu kiasi cha kufikia kuwaua wananchi wake ambao wanadai haki zao, kwa mfano wananchi walio uwawa katika maandamano yaliyofanywa na chama pinzani huko Arusha, pia kupanda kwa gharama za maisha, hali ngumu ya uchumi, huduma mbovu za kijamii ambazo zinadhirika pale tunapowaona wananch wakikimbilia kijijini Samunge kupata kikombe cha babu, hili linaonesha wazi hali ngumu na ubovu wa huduma tunazopatiwa, haina maana kuwa watu wanapenda wote kwenda kupata kikombe cha babu bali hawana kimbilio baada ya serikali kutotimiza wajibu wake wa kuwahudumia wananchi ipasavyo. Hata hivyo kwa mtazamo wangu, mimi sioni faida ya kutumia mamilioni ya fedha kuandaa sherehe itakayofanyika kwa siku moja na huku wananchi wanateseka kwa kukosa mahitaji muhimu, wakati huohuo viongozi tuliowapa madaraka wanang'ang'ania kujilimbikizia mali na kudai posho kila wakati, hivyo ni bora fedha hizo ya posho nakiasi fulani kutoka katika mfuko huo wa maandalizi ya sherehe za uhuru zikawekwa katika maendeleo ya jamii na wanajamii hushka.

Mtazamo: Kamajitihada za makusudi hazitachukuliwa kuinusuru hali iliyopo,
tunalichimbia taifa letu kaburi ambalo hatutampata wa kutusaidia, inawezekana
tukaingia katika mgogoro na maandamano kama ilivyo kwa nchi kama Ivory
coast, Tunisia na nchi nyingine za kiislam.
Wito wangu kwa serikali
na wanasiasa ni kuwa, miaka hamsini
ya uhuru wa Tanzania si lolote si chochote kama hauendani na mahitaji ya
wanajamii wa Tanzani. Hata hivyo nawaomba waache kuchanganya siasa na utendaji
wa shughuli za maendeleo la sivyo watakuwa wanataka kuwasha moto usio na
wakuuzima.
Naipenda nchi yangu, nawapenda watu wake, Mungu ibariki Tanzania,
Mungu ibariki afrika
No comments
Thank for your coment