"BORA KINGA KULIKO TIBA"

Ni hivi karibuni tu tumekuwa tukisikia huko kwa wenzetu au jirani zetu Kenya kuwa kwa sasa wanakabiliwa na tatizo kubwa la upungufu wa wa kinga kama wanavyoita wengi, ndomu au kwa vijana ili kuficha maana huita dawa ya penzi kwa jina lake maarufu KONDOM.
Hili kwa jirani zetu limekuwa tatizo ambalo hadi sasa imefikia hatua ya mtu anapotumia kondom inabidi aifue kwa matumizi ya baadae au hadi wengine kufikia kutumia mifuko ya plastic kama njia mbadala.
Hii ni hali mbaya ambayo haivumiliki, ni hatari kwa wananchi na jamii nzima kwa ujumla.
Hata hivyo mtu aweza kujiuliza maswali kadha.
Hivi kweli matumizi ya Kondomu ni kinga halisi kwa magonjwa ya kuambukiza yatokanayo na ngono zikiwemo mimba zisio tarajiwa? Ni hatari gani yaweza kutokea endapo kunakuwa na upungufu au ukosefu wa Kondom? Ina maana kuwa Kenya ndo wanajali zaidi kuliko wengine? Au wao ndio wanaoongoza kwa kufanya ngono? Haya na mengine megi husumbua vichwa vya wengi. Pengine ni kweli wanajali kwani takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya ukimwi kimepungua kutoka asilimia 15 hadi 6.5, bila shaka hizi ni jitihada za hali ya juu kwa serikali, ila pia hebu tujiulize kuwa hivi ni nani hasa mlengwa wa Kondom? Watoto, Wazee, rika la Makamo au Vijana? Hili bado ni tatizo pia kwani kiuhalisia vijana ndo wanaongoza kwa matumizi ya Kondom.
Kama takwimu zioneshavyo kwa Mkoa mmojatu nchini humo unahitaji Kondom milioni ishirini kwa mwezi, taifa zima kinahitajika kiasigani?
Tumeona jitihada za kuomba misaada kutoka nje zinafanyika na kwa bahati nzuri wahisani wameahidi kuipatia Kenya Kondom milioni 30 kwa mwezi kuanzia mwezi Mei hadi Agost, na kutokana na ukubwa wa tatizo serikali ya Marekani imeahidi kuipatia Kenya Kondomu milioni 45 kwa mwezi, ni msaada wa hali na mali kunusuru wananchi. Ila hivi mpaka lini hitakwisha?!...
Hili tumeliona kwa wenzetu kwetu halipo? Sisi ni waaminifu sana? Tumepata elimu ya kutosha hivyo tumeamua kusubiri? Au sisi ndo hatujui umuhimu wa kujikinga na maambukizi ya Ukimwi kwa kutumia Kondom hivyo tunafanya ngono pasipo kinga?
Tumekuwa tukishuhudia kampeni mbalimbali kuhusu mapambano dhidi ya Ukimwi ikiwemo aliyoanzisha Raisi wetu ndugu Jakaya Kiwete ya "Tanzania bila Ukimwi inawezekana" hongera sana mheshimiwa, pia zipo asasi mbalimbali zisizo za kiserikali pia zinahitaji pongezi.
Ila nasi tungefurahi endapo tungepata takwimu kuhusu matumizi na uhitaji wa kondom katika nchi yetu na kama kuna upungufu au la na kama upo ni jitihada gani zinafanyika.
Yawezekana kwa waishio mijini wasilione tatizo hili, ila kwa wanaoishi pembezoni mwa nchi huwa wanakumbana nalo, je serikali na wadau mnachukua hatua gani? Isije kuwa kwetu lipo tatizo zaidi kuliko jirani zetu.
Mwenzio akinyolewa wewe suka au tia maji, na ni bora kinga kuliko tiba.

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.