UCHAGUZI WA SERIKALI YA WANACHUO UDOM.

Ni harakati za kuwachagua viongozi wa serikali ya chuo kikuu Cha Dodoma ambao ulipangwa kuanza tarehe 06,May.2011 kwa kuwachagua wabunge, wawakilishi wa wanachuo, na viongozi wa blocks, uchaguzi huo uliahirishwa kutokana na msiba wa mwanachuo mwenzao wa mwaka wa kwanza, hata hivyo uchaguzi huo uliambatanishwa na uchaguzi wa raisi wa chuo kizima, serikali ya federation na maraisi wa collages mbalimbali ulipangwa kufanyika tarehe 07, May. 2011.

Hata hivyo uchaguzi huu ulizongwa na zemgwe nyingi kutokana na mapungufu mengi yaliyo onekana kutokea ikiwemo maandalizi mabovu yaliyo ambatana na uongozi mbovu kutokana na baadhi ya wapiga kura kukosa majina yao katika vituo vyao pia likiwemo swala la wanachuo wanaochukua shahada ya pili (MASTERS) kutoruhusiwa kupiga kura jambo ambalo lilizua gumzo na maswali mengi ikiwemo swali kuwa masters wao wanachukuliwa kama nani chuoni hapa iwapo hawana haki ya kuwachagua viongozi wa serikali ya chuo chao, pia walihoji sababu za kutohusishwa katika uchaguzi huo wakati hata wao wanachangia fedha za UDOSO tena zaidi ya hawa wanaochukua shahada ya kwanza ambapo wao wao hutoa shilingi 20000/= ilhali wengine hutoa 5000/= tu.

Mapungufu hayo pamoja na mengine mengi yamekuwa ni kero na kuwafanya watu kuhisi kuwepo kwa aina fulani ya zengwe linalotakiwa kuchezwa kutokana na ushindani mkubwa kati ya wagombea hasa katika nafasi ya raisi koleji ya sayansi za jamii kati ya bwana MWAKIBINGA PHILIPO na GODWIN GONDE. Hata hivyo hadi tuna ingia mitamboni bado zoezi la upigaji kura lilikuwa likiendelea vizuri pamoja nakuwapo mapungufu memgi.

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.