HAPPY NEW YEAR "2012"

Ni mwaka mpya, mwaka ambao wengi tulikuwa tunausubiri kwa hamu, mwaka ambao kwanza ni mchanga, ikiwa leo ndoyo siku ya pili ya mwezi wa kwanza katika mwaka wa 2012, sote hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kutufikisha, hapa tukiwa wazima wa afya kila mmoja kwa nafasi yake.


Pia hatuna budi kutafakari yale tuliyotenda katika mwaka uliopita, yale yaliyokuwa mema tuyaenzi, na mabaya kuyatupilia mbali, kuangalia mafanikio na mapungufu tuliyokuwa nayo yaliyopelekea kutofikia malengo tuliyokuwa tumejiwekea, yote ikiwa ni lengo la kuleta ufanisi katika utendaji wetu wa kazi.


Hata hivyo katika maka huu uliopita tumewapoteza ndugu zetu wengu kutokana na matulio mbalimbali, kama vile ajali za barabarani, magonjwa, na vurugu za kisiasa pia yakiwemo matukio makubwa ambayo yalilitikisa taifa ambayo ni milipuko ya mabomu katika kambi ya jeshi Gongolamboto, ajali ya Meli MV SPICE ISLANDER pamoja na mafuriko ambayo yamekumba baadhi ya maeneo katika jiji la Dar es Salaam. Sote kwa pamoja hatunabudi kuungana na kuwaombea ndugu zetu waliotangulia mbele ya haki ili wapate pumziko la milele.


Hata hivyo pia wapo ndugu zetu ambao mwaka mpya umewakuta wakiwa katika hali ya kuumwa wakiwemo hospitalini na hata nyumbani kwao, pia kwa pamoja tunapaswa kuwaombea ili wapate kupona mapema na kujiunga na familia, ndugu, jamaa na rafiki zao katika harakati za ujenzi wa taifa.


Pia tunapaswa kujua kuwa mwaka mpya sio kukaa, kusherehekea na kukusanyika na familia zetu, bali kujipanga upya ili kuhakikisha kuwa tunafikia malengo tuliyojiwekea katika maisha yetu.
Hivyo basi ni fursa kila mmoja wetu kuhakikisha kuwa anajiwekea malengo yake ambayo kwayo itakuwa ndiyo nguzo ya msingi katika utendaji wake wa kazi.


HERI YA MWAKA MPYA "2012" WENYE BARAKA NA MAFANIKIO

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.