PEDRO VERONA ASHINDA TUZO YA MO IBRAHIM

Aliyekuwa Rais wa Visiwa vya Cape Verde Pedre Verona Pires ashinda tuzo ya Mo Ibrahim ya utawala bora barani Afrika.


Tuzo hiyo inathamani ya dola milioni tano (5 mil) katika kumi ya utawala wake na dola 200,000 katika kipindi chote maisha yake.


Kamati inayohusika na utoaji wa tuzo hiyo imesema kuwa Pedro Verona aliisaidia sana nchi yake na kuifanya kuwa mfano mzuri na wa kuigwa wa utawala bora wa kidemokrasia, kuwepo kwa uhuru binafsi, kuheshimu na kulinda haki za binadam, msimamo wa kisiasa na maendeleo ya kiuchumi.


Pedro Verona kabla ya kustafu alikataa kubadilisha katiba ya inchi hiyo ili kumuwezesha kugombea uraisi tena baada ya kumaliza kipindi chake cha miaka kumi tofauti na maraisi wengine barani Afrika ambavyo wamekuwa wakifanya.


Tuzo hii ya Mo Ibrahim imeanzishwa mwaka 2006 na bilinea wa Sudan 'MO IBRAHIM' ambapo kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita tuzo hii haikutolewa kutokana na kukosekana kwa maraisi wenye vigezo vya kushinda tuzo hii.


Raisi Pedro Verona ambaye ana umri wa miaka 77 ametumia miaka hamsi ya maisha yake katika siasa ambapo mnamo mwaka 1975 aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo, mwaka 1991 aliingia katika kinyang'anyiro cha uraisi ambapo alishindwa, na mwaka 2001 alishinda na kuwa Raisi wa kisiwa hicho na mwaka 2006 akashinda awamu ya pili ya uraisi.


Hata hivyo sisi tunatakiwa kujiuliza kuwa Tanzania imekuwa na Maraisi wangapi na kwanini asiwepo hata mmoja wa kushinda tuzo hii?... Tuzo hii inatoa funzo gani kwa maraisi wa kiafrika?.... Je wananchi wenyewe wa nchi za kiafrika wanaonaje kuhusu tuzo hii?


Sote hatunabudi kutafakari na kuchukua hatua madhubudi.

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.