Tuwathamini Mashujaa wa kweli na sio wa Vyeo



 Huwa ni kawaida na mazoea ya jamii, watu binafsi, asasi za kiraia, mashirika yasiyo ya kiserikali na sehemu mbalimbali kutoa zawadi kwa wale wanaoonekana kuwa na mchango au kuwa na jitihada katika utendaji wa kazi na umakini katika kufanya kazi wanazopewa.


Hata hivyo wakati mwingine tumeshuhudia zawadi hizo zikitolewa kwa kijuana, au kwa ahadi ya kurudisha fadhila kwa anayekupa zawadi hiyo.


Wakati mwingine zawadi hizo hutulewa kwa watu wasiokuwa na sifa za kupewa zawadi.


Jamii imewasahau nakutowajali wale ambao zawadi hizo ni halali kwao.


Hebu tujiulize kuwa nilini jamii ilikaa na kuamua kuwapa zawadi akina mama ambao wamekuwa wakifanya kazi kubwa katika familia zao, hufanya kazi ngumu ya kuilea jamii ili iwe na mwelekeo mzuri.


Pia kuna kundi wa wazee (babu na bibi zetu) ambao kwa mara nyingine jamii inawapa jukumu zito la kuwalea wajukuu kwa kisingizio kuwa tunayatafuta maisha.


Lakini hatujawahi kusikia kiwa wazee hao wanaandaliwa zawadi kwa kazi kubwa wanayoifanya, hili linasikitisha na kutia huruma hasa tunapo shuhudia sisi tunao wabebesha mizigo hiyo tunamua kupeana zawadi wenyewe bila hata kuwafikiria wazee wetu waliotulea na sasa tunawapa kazi ya kulea wajukuu.


Inatupasa tubadilike na kuona umuhimu wa kutoa zawadi kwa wastahili wa zawadi hizo na kupeana zawadi kisa tunajana kwa vyeo vyutu.

No comments

Thank for your coment

Powered by Blogger.