"ASANTE SANA AUNT"
Wewe ni moja kati ya watu ambao mimi naweza kusema kuwa ni wa ajabu na wapekee sana katika ulimwengu huu, mtu ambaye kila mwenye uwezo wa utambuzi basi heshu kukuelezea, si kwa ubaya bali utofauti kati yako na watu wengine.
Ninapenda niuelezee umahiri, uzuri,umuhimu na thamani yako katika maisha yangu.
Umekuwa msaada wa hali na mali kwangu na bila ya shaka sitakuwa mkosefu endapo nitasema "isingekuwa wewe," nisingefika hapa nilipo leo hii, japo sijasimama kwa miguu yangu mwenyewe ila nautambua na kuuthamini mchango wako kunifanya mimi kuwa mimi wa leo hii, umenipa mwongozo na kunifanya nisikate tamaa, mawazo yako ni taa tosha katika njia zangu, umenipenda na kunijali pia kunifanya mmoja ya wana wa familia yako pasi kujali undugu, ujamaa au hata ujirani.
Kupitia kwako nimeuona upendo wa mama, sikuhisi tofauti yoyote wala upweke kwani nimekuwa sehemu ya familia, kipindi chote nilipokuwa nikifanya shughuli zangu hasa za kielimu, nimeishi na wewe kwa amani na upendo pasi kukasirika au kupata manyanyaso ya aina yoyote, nimekaa na ndugu zangu pasipo kufarakana au misukosuko ya aina yoyote, ndio maana napenda nikushukuru kwa uhisani wako ndugu zako na familia yako kwa ujumla akiwemo dada Nakija Mteti, Shakila Mohamed, Hasani Mohame, Zai mkubwa, Zainabu Dhahir, Neema Mohamed, na Rafiki yangu kipenzi na ndugu yangu wa pekee AMOS ALISON MWAISABILA. Nawapenda sana wote, natambua uwepo na mchango wao kwangu.
Hata hivyo vikombe kabatini hutokea wakati vikagongana, hivyo, huenda katika mahangaiko imetokea aidha kwa bahati mbaya nikafanya kinyume na matarajio au nikawa nimekosea pasipo kujua au hata kwa kukosewa pia, hivyo kwa hali ya ubinadamu kukosa tumeumbiwa. Kwa moyo wa unyenyekevu naomba kwa yoyote niliyemkosea aniwie radhi na tuzidisha udugu wetu kama familia moja sasa ili tuweze kuyafikia malengo yetu.
Nakupenda sana Aunt, na ninamuomba Mungu akuzidishie roho ya ukarimu, upendo, ujasiri, huruma, na unyenyekevu, akuzidishie katika kipato chako (uime thathi ishi na ugure mbane pithi, kadori kaoke kabaha) ili uwasaidie na wenye uhitaji kama ilivyokuwa kwangu.
Pia namwomba mungu amjalia ndugu yangu, kaka yangu, mdogo wangu mpendwa "Amos" afya njema na maisha marefu, heri na fanaka katika masomo yake.
Ni mimi mwanao katika familia bora. Finland Bernard.
No comments
Thank for your coment