HIVI NDIVYO KATIBU MKUU WIZARA YA NISHATI NA MADINI ALIVYOOMBA RUSHWA
Barua ambayo aliiandika katibu mkuu wizara ya nishati na madini Ndg David Jairo |
Ni hivi karibuni tumeshuhudia kuahirishwa kwa bajeti ya wizara ya nishati na madini baada ya kubainika uozo iliokuwa umejificha ndani yake, hili limetokea baada ya katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini ndugu DAVI JAIRO kuandika baruka kwa taasisi zaidi ya ishirini kuomba fedha kiasi cha Tsh 50,000,000/= kwa kila taasisi ili kuwezesha uwasilishwaji wa bajeti ya wizara hiyo.
Swala hili limezua gumzzo katika maeneo mbalimbali kuanzia kwa wbunge wenyewe hadi kwa wananchi ambapo wananchi wanachohitaji ni wizara nzima kuachia ngazi na hatua za kinidham kuchukuliwa dhidi yao.
Hata hivyo serikali imeomba wiki tatu ili kufanyia utaratibu bajeti hiyon na kuirudisha tena bungeni baada ya wiki hizo tatu, kutokana na tukio hilo wnanchi na wasomi mbalimbali na wabunge wa kambi ya upinzani wa wanadai kinachotakiwa ni bajeti nzima kurudiwa kwani inaonesha kuwa japo hili limetokea katika wizara moja, inawezekana lipo pia katika wizara nyingine.
Kufuatia tukia hili waziri mkuu Mh: Mizengo Pinda alidai ni kwavile hana uwezo wa kumuwajibisha moja kwa moja kwa kwa kumfukuza kazi hivyo anasubiri kauli kutoka kwa mheshimiwa Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
taarifa zisizo rasmi zinadai kuwa tayari katibu mkuu huyo amekwisha achia nafasi yake na kupisha utaratibu mwingine kuchukua nafasi dhidi yake.
No comments
Thank for your coment